Social Icons

Jumatano, 26 Machi 2014

YAFAHAMU MAZAO YA NYUKI NA MATUMIZI YAKE


Mzao makuu ya nyuki ni pamoja na asali, nta, chavua, gundi ya nyuki na sumu ya nyuki.
ASALI (HONEY)
Asali hutengenezwa na nyuki kwa ajili ya chakula cha akiba.
Asali hutokana na maji matamu anayochukua nyuki kutoka kwenye maua. Wakati nyuki akikusanya maji hayo matamu yanakuwa na asilimia 20-40 ya sukari. Asilimia iliyobaki ni maji.

Asilimia hizo hupunguzwa au kuongezwa na nyuki akitumia madawa yatokayo kwenye matezi yake. Asali iliyoiva ina sukari asilimia 75-85 na maji asilimia 17-20.
Asali hutofautiana rangi, ladha vinyumbulisho kutegemeana na aina za maua aliyotembelea.
Faida za asali ni pamoja na matumizi ya nyumbani kama lishe, hutumika kama dawa pia kuboresha kipato cha mfugaji nyuki. Asali ni dawa kwa magonjwa mengi .


image.jpeg

NTA (BEESWAX)
Nta ni zao la nyuki litokalo katika mwili wa nyuki kwenye matezi yaliyopo katika sehemu ya chini ya tumbo la nyuki kibarua. Halitoki kwenye mimea kama wengi wanavyofikiria.
Kabla ya kutoa nta nyuki kibarua hutakiwa kula asali na kukaa kwa muda wa masaa 24. Matezi hutoa nta ambayo hukusanywa kwa kupelekwa mdomoni kutafunwa / kufinyangwa na kutengenezwa masega. Faida kubwa za zao la nta ni kuongeza kipato cha mfugaji nyuki kwa kuuza zao lenyewe na bidhaa zitokanazo na matumizi ya nta kama mishumaa, polishi ya samani, viatu na kadhalika.

image.jpeg

CHAVUA (POLLEN)
Chavua ni zao la nyuki kutoka kwenye mimea na ni chakula kinachompatia nyuki protein. Nyuki hukusanya chavua anapotembelea maua. Chavua hujishikiza kwenye vinyweleo vyake vya mwilini na sehemu za miguuni. Chavua hukusanywa kutoka kwenye vinyweleo vya mwili kwa miguu ya mbele hadi kufikia miguu ya nyuma yenye kipepeo. Mahitaji ya kundi la nyuki ni kama kiligram 35-40 za chavua kwa mwaka kutokana na ukubwa wa kundi la nyuki. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni