Bumba la nyuki hupatikana sehemu zenye giza na mara chache sehemu za wazi. Bumba la nyuki hutengenezwa kwa masega yenye nyumba (cells). Kuna nyumba kwa ajili ya kuangulia nyuki vibarua, nyuki dume na malkia. Vyumba kwa ajili ya kuangulia nyuki vibarua na madume vimetengenezwa kuwa na kuta sita na vya malkia ni kama mfano wa duara ndani.
Masega hutengenezwa kutokana na nta inayotayarishwa katika matezi ya nyuki kibarua baada ya kula asali. Kwa kawaida katika kiota cha nyuki wanaweza kuwepo idadi ya nyuki 50,000 - 100,000. Wengi wao ni nyuki vibarua.
Utagaji wa mayai huanza katikati ya sega kwa mfano wa duara. Upande wa juu wa sega huhifadhiwa chavua na sehemu ya chini ya sega huhifadhiwa asali
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni