Social Icons

Ijumaa, 28 Machi 2014

YAFAHAMU MATUMIZI YA CHAVUA MATUMIZI YA CHAVUA, SOMA HAPA

image.jpeg

MATUMIZI YA CHAVUA
  • Chavua inatumika kama chakula cha binadamu.
  • Chavua ina virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na
    protini, mafuta, vitamini A na B pamoja na madini aina mbalimbali.
    Njia nzuri ya kutumia chavua ni ile ya kuitafuna ichanganyike na mate. Kama ladha haipendezi ichanganye na maji, maziwa au asali.
    FAIDA YA CHAVUA KIAFYA
    1. Kuongeza hamu ya kula.
    2. Huponyesha misokoto ya tumbo.
    3. Husaidia mwili kukua (kujenga mwili).
    4. Husaidia kukuza nywele.
    5. Huongeza uwezo wa kuona.
    6. Hutibu magonjwa ya moyo.
    7. Hufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa rahisi na

    mwepesi.
    8. Hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. 9. Hutibu magonjwa ya kiume kama vile ngiri.

 GUNDI YA NYUKI (PROPOLIS)
UFUGAJI NYUKI
Hii ni zao la nyuki litokanalo na utomvu wa miti. Nyuki hutumia zao hili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ndani ya mzinga, kuimarisha masega, kuwadhibiti maadui.
Kwa binadamu hutumika kama dawa. Pia kuongeza kipato cha mfugaji nyuki baada ya kuuza zao hili. Gundi ya nyuki ina thamani kubwa sana.

Picha ya nyuki anayekusanya na kubeba chavua 


SUMU YA NYUKI (BEE VENOM)
Sumu ya nyuki huhifadhiwa ndani ya mfuko maalum kwenye mwili wa nyuki Kibarua. Huitoa nje kutumia mwiba wa kuuma. Nyuki kibarua mchanga huwa na sumu kidogo na jinsi anavyokuwa sumu huongezeka. Nyuki kibarua akifikia umri wa siku 18 sumu haiongezeki tena na huu ndio umri wa ulinzi wa ndani na nje ya mzinga. Nyuki akishatoa sumu, hiyo hawezi tena kuirudisha kwenye mfuko huo wa kuhifadhia kwani sehemu atumiazo nje zikiambatana na misuli na mfuko wa kuhifadhia sumu.
Nyuki huitoa sumu nje kwa kutumia mwiba anapomshambulia adui. Baada ya kuutoa mwiba nje na kubakia sehemu ya shambulio hufa baada ya masaa machache.
MATUMIZI YA SUMU YA NYUKI
Sumu ya nyuki hutumika kutibu baadhi ya magonjwa kama maumivu ya uvimbe / magonjwa ya viungo na kadhalika.
UBORA WA MAZAO YA NYUKI
Nchini wamejitokeza wafanyabiashara wengi wanaosafirisha mazao ya nyuki nje ya nchi. Kwa kufanya hivyo hupata fedha za kigeni. Biashara ya mazao haya inaweza kufanikiwa zaidi kama yatakuwa katika hali ya ubora.
MATUMIZI YA NYUKI KWA AJILI YA UCHAVUSHAJI (POLLINATION)
Nyuki anapotembelea maua ili akusanye chakula katika mimea/miti aina mbalimbali huchavusha kwa kutoa mbegu za kiume za ua na kusambaza kwenye mbegu za kike za ua la aina hiyohiyo yatokanayo na kitendo hiki huwa ni bora, imara na mengi.
Uchavushaji huu pia husaidia kuhifadhi mazingira baada ya mbegu hizo bora na nyingi kusambazwa maeneo yaliyoathirika (yasiyo wazi) kwa njia ya upepo, maji, wanyama na kadhalika na kuendeleza uoto au kuanzisha uoto mpya. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni