Social Icons

Jumatatu, 17 Februari 2014

JE UNAJUA KWA NINI TUNAFUGA NYUKI, SOMA HAPA KUPATA UFAHAMU -SEHEMU YA PILI






AINA ZA NYUKI

Nyuki wamegawanyika katika makundi makuu mawili: yaani nyuki wajamaa na nyuki waishio upweke. Nyuki wajamaa ndio wa asali na nta na ni muhimu kwa mfugaji nyuki.

Aina mbili kuu za nyuki ni:
1. Nyuki wasiouma
2. Nyuki wanauma.

NYUKI WASIOUMA:

Kabila kuu tatu za nyuki wasiouma ni:
(i) Nyuki wakubwa kwa umbile weusi na huweka asali katika nyungu. Kila kabila lina jina la asili hii ya nyuki kwa mfano Nyori- Chaga, Hongwa-Ndengereko.
(ii) Nyuki wenye umbile la kati weusi, na hupenda kujenga katika mapango ya miti iliyooza na kuweka asali kwenye vyungu vidogo.
(iii) Nyuki wasiouma wenye tabia ya kujenga chini ya ardhi.

NYUKI WANAOUMA:

Aina hii ya nyuki hutofautiana kutokana na umbile, maeneo, rangi na tabia. Hapa nchini tunao kabila kuu tatu kama ifuatavyo:

Nyuki wa milimani - Apis mellifera monticola Nyuki wa tambarare - A. M menticola
Nyuki wa pwani - Apis mellifera liforea

Nyuki wa milimani:
Nyuki waishio nyanda za juu, weusi, wakubwa kuliko nyuki wa tambarare na pwani, wapole na hawana tabia ya kuweka akiba ya asali nyingi.

Nyuki wa tambarare:
Umbile lao ni la kati, sio wakali sana na huwa na tabia ya kuweka asali nyingi.

Nyuki wa pwani:
Ni nyuki wenye umbile dogo na wana tabia ya kuhifadhi akiba ya asali nyingi.

Nyuki hawa wana ushirikiano mkubwa sana katika harakati za maisha. Wanamgawanyo wa kazi kutokana na maumbile kama ifuatavyo: 
malkia, vibarua na dume.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni