Social Icons

Alhamisi, 27 Machi 2014

SOMO MUHIMU LA LEO: JINSI YA KUPATA MAZAO BORA YA NYUKI ASALI (HONEY):




Ili kudumisha ubora wa asali mfugaji nyuki/msindikaji asali anatakiwa kuzingatia yafuatayo:
Kupata asali safi:
  1. a)  Zingatia kalenda ya ufugaji nyuki.
  2. b)  Vuna asali isiyo na chavua.
  3. c)  Vuna asali iliyokomaa.
  4. d)  Wakati wa kuvuna tumia zana za kinga.
  5. e)  Tumia vyombo vya plastiki, glasi vilivyo visafi na
    vyenye mifuniko imara.
  6. f)  Unapovuna tumia kisu kukata masega (usisahau
    kuachia nyuki robo ya mavuno ndani ya mzinga) na
    hakikisha nyuki wamepanguswa kwenye sega.
  7. g)  Hifadhi asali iliyovunwa sehemu isiyo na unyevu
    nyevu au joto kali.
UFUGAJI NYUKI
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA UVUNAJI WA ASALI
  • Usisimame katika njia wanayotumia nyuki yaani mbele
    ya mlango wa mzinga.
  • Usipakue asali wakati wa joto, jua kali au wakati mvua
    ikinyesha.
  • Unapovuna asali hakikisha umevaa mavazi ya kinga
    pia andaa zana za kumhudumia nyuki kama bomba la
    moshi.
  • Fanya kazi kwa utulivu bila ya kelele ya aina yeyote.
  • Fanya kazi kwa haraka lakini kwa uangalifu.
  • Tumia bomba la moshi kufukiza moshi ndani ya mzinga
    kwa uangalifu kisha fukiza moshi juu ya viunzi ndani ya
    mzinga.
  • Ondosha kiunzi au viunzi vichache vilivyo tupu ili
    kuweka uwazi mwishoni mwa mzinga upande mmoja. Kitendo hiki kisiwabughudhi nyuki na anza kusogeza kiunzi kimoja kimoja kwa lengo la kukagua au kuvuna asali na endelea kutumia bomba la moshi.
  • Hakikisha unarudisha kiunzi kama kilivyokuwa katika mzinga bila ya kuwadhuru nyuki.
  • Mwisho kabisa kwa taratibu rudisha mfuniko juu ya mzinga. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni