Social Icons

Featured Posts

Alhamisi, 5 Juni 2014

FUGENI NYUKI KUONDOKANA NA UMASIKINI‏



Na Samwel Mwanga-Maswa
 
WANANCHI  wameshauriwa kufuga nyuki ili waweze kujiongezea kipato na
kuwainua kiuchumi na hivyo kuondokana na umasikini kwa kuwa ufugaji
huo ni moja ya shughuli za maendeleo.
 
Ushauri huo umetolewa  jana na Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Mradi
wa Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira ya Ziwa Victoria(LIVEMPII),Paul
Kariuki mara baada ya kutembelea Mradi wa Ufugaji nyuki katika kijiji
cha Ipililo wilayani Maswa mkoani Simiyu.
 
Alisema kuwa fursa hiyo waliyoipata ni nzuri na hivyo ni vizuri
wakaitumia kwa uzalishaji kuliko kutegemea kila kitu watafanyiwa na
serikali ili waweze kuondokana na umasikini kwa wananchi hasa waishiyo
maeneo ya vijijini.
 
“Umasikini sasa basi ndugu zangu wananchi hasa wa hapa Ipililo mseme
kuwa umasikini mmeanza kuuaga kuanzia hapa kutokana na ufugaji wa
nyuki ambao unafaida kubwa kwani tunaweza kupata asali pamoja na Nta
ambazo  zina bei kubwa kulingana na mahitaji yake ”alisema.
 
Kariuki ambaye aliambatana na wakulima na wataalam mbalimbali wa
mazingira kutoka nchini Kenya waliokuwa katika ziara ya siku tatu
wilayani Maswa kutembelea Miradi ya LIVEMP II Wilayani humo alisema
kuwa wafugaji nyuki pia husaidia kuhifadhi mazingira.
 
 “Ufugaji wa nyuki huhifadhi mazingira kwani kwa kutundika mizinga ya
nyuki  kwenye misitu  wanakijiji  wanashindwa  kuvamia misitu hiyo na
wale wavamizi wakorofi wanaovamia misitu hiyo hukabiliana na nyuki kwa
kuumwa”alisema.
 
Awali akisoma taarifa ya Mradi huo unaofadhiliwa na LIVEMP II,Ofisa
Kilimo wa Kata ya Ipililo,Inocent Kavela alisema kuwa kutokana na
mizinga waliyonayo 185 iliyotundikwa wanatarajia kuvuna kiasi cha kilo
2500 za asali na Nta kilo 278.
 
‘Matarajio ya uvunaji wa mazao ya nyuki tunategemea kuvuna kiasi cha
Kilo 2500 na Nta kilo 278 na katika soko la sasa bei ya kilo moja ya
Sali ni shilingi 10,000/= hadi 12,000/= na Nta ni shilingi 15,000/=
hadi 25,000/= kwa kilo”Alisema.
 
Mradi wa ufugaji wa nyuki katika kijiji cha Ipililo unawahusisha
wanakikundi wapatao 27 kati yao wamawake 11 na wanaume 16 na kiasi cha
Shilingi 30,914,600/= zimetolewa na LIVEMP II kuutekeleza kwa kipindi
cha Mwaka 2013/2014.

Ijumaa, 23 Mei 2014

FAHAMU MATUMIZI YA ASALI KWA UPONYAJI WA MISHONO YA OPERATION.

 

ASALI ni dawa nzuri sana katika kutibu mishono ya operation mbali mbali. Wataalamu wanazidi kuhamasisha matumizi ya asali kwenye mishono kila siku.
Asali Imekua inatumika kwa miaka mingi kwasababu zifuatazo:-

1. Ina kiwango kikubwa cha sukari ( High Sugar content) inayofanya bakteria washindwe kuzaliana au kuishi.

2. Ina kiwango kidogo cha unyevu ( Low Moisture content) - hii inafanya kidonda kiwe kikavu

3. Ina HYDROGEN PEROXIDE ambayo inazuia bakteria

4. Gluconic acid ambayo inatengeneza mazingira ya Acid kwenye kidonda na hivyo kuzuia ukuaji wa bakteria.

Faida ya kutumia ASALI kwenye mishono ya operation ni pamoja na:-

1. Inapunguza kuvimba kwa kidonda na pia uvimbe wa kidonda

2. Inaongeza spidi ya uponaji wa kidonda.

3. Inasafisha kidonda

MATUMIZI YAKE
Unaweza paka hadi mara mbili kwa siku kuharakisha uponaji, lakini hakikisha asali hiyo ni safi.

ANGALIZO
Unashauriwa upate ushauri wa kitaalamu kwanza wa daktari wako kabla ya kujiamulia kupaka mwenyewe nyumbani ili kufanya kitu sahihi.

Tafadhali naomba TUSHARE kwa wingi sana ili watu wengi waipate elimu hii.

Ijumaa, 28 Machi 2014

YAFAHAMU MATUMIZI YA CHAVUA MATUMIZI YA CHAVUA, SOMA HAPA

image.jpeg

MATUMIZI YA CHAVUA
  • Chavua inatumika kama chakula cha binadamu.
  • Chavua ina virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na
    protini, mafuta, vitamini A na B pamoja na madini aina mbalimbali.
    Njia nzuri ya kutumia chavua ni ile ya kuitafuna ichanganyike na mate. Kama ladha haipendezi ichanganye na maji, maziwa au asali.
    FAIDA YA CHAVUA KIAFYA
    1. Kuongeza hamu ya kula.
    2. Huponyesha misokoto ya tumbo.
    3. Husaidia mwili kukua (kujenga mwili).
    4. Husaidia kukuza nywele.
    5. Huongeza uwezo wa kuona.
    6. Hutibu magonjwa ya moyo.
    7. Hufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa rahisi na

    mwepesi.
    8. Hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. 9. Hutibu magonjwa ya kiume kama vile ngiri.

 GUNDI YA NYUKI (PROPOLIS)
UFUGAJI NYUKI
Hii ni zao la nyuki litokanalo na utomvu wa miti. Nyuki hutumia zao hili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ndani ya mzinga, kuimarisha masega, kuwadhibiti maadui.
Kwa binadamu hutumika kama dawa. Pia kuongeza kipato cha mfugaji nyuki baada ya kuuza zao hili. Gundi ya nyuki ina thamani kubwa sana.

Picha ya nyuki anayekusanya na kubeba chavua 


SUMU YA NYUKI (BEE VENOM)
Sumu ya nyuki huhifadhiwa ndani ya mfuko maalum kwenye mwili wa nyuki Kibarua. Huitoa nje kutumia mwiba wa kuuma. Nyuki kibarua mchanga huwa na sumu kidogo na jinsi anavyokuwa sumu huongezeka. Nyuki kibarua akifikia umri wa siku 18 sumu haiongezeki tena na huu ndio umri wa ulinzi wa ndani na nje ya mzinga. Nyuki akishatoa sumu, hiyo hawezi tena kuirudisha kwenye mfuko huo wa kuhifadhia kwani sehemu atumiazo nje zikiambatana na misuli na mfuko wa kuhifadhia sumu.
Nyuki huitoa sumu nje kwa kutumia mwiba anapomshambulia adui. Baada ya kuutoa mwiba nje na kubakia sehemu ya shambulio hufa baada ya masaa machache.
MATUMIZI YA SUMU YA NYUKI
Sumu ya nyuki hutumika kutibu baadhi ya magonjwa kama maumivu ya uvimbe / magonjwa ya viungo na kadhalika.
UBORA WA MAZAO YA NYUKI
Nchini wamejitokeza wafanyabiashara wengi wanaosafirisha mazao ya nyuki nje ya nchi. Kwa kufanya hivyo hupata fedha za kigeni. Biashara ya mazao haya inaweza kufanikiwa zaidi kama yatakuwa katika hali ya ubora.
MATUMIZI YA NYUKI KWA AJILI YA UCHAVUSHAJI (POLLINATION)
Nyuki anapotembelea maua ili akusanye chakula katika mimea/miti aina mbalimbali huchavusha kwa kutoa mbegu za kiume za ua na kusambaza kwenye mbegu za kike za ua la aina hiyohiyo yatokanayo na kitendo hiki huwa ni bora, imara na mengi.
Uchavushaji huu pia husaidia kuhifadhi mazingira baada ya mbegu hizo bora na nyingi kusambazwa maeneo yaliyoathirika (yasiyo wazi) kwa njia ya upepo, maji, wanyama na kadhalika na kuendeleza uoto au kuanzisha uoto mpya. 

Alhamisi, 27 Machi 2014

SOMO MUHIMU LA LEO: JINSI YA KUPATA MAZAO BORA YA NYUKI ASALI (HONEY):




Ili kudumisha ubora wa asali mfugaji nyuki/msindikaji asali anatakiwa kuzingatia yafuatayo:
Kupata asali safi:
  1. a)  Zingatia kalenda ya ufugaji nyuki.
  2. b)  Vuna asali isiyo na chavua.
  3. c)  Vuna asali iliyokomaa.
  4. d)  Wakati wa kuvuna tumia zana za kinga.
  5. e)  Tumia vyombo vya plastiki, glasi vilivyo visafi na
    vyenye mifuniko imara.
  6. f)  Unapovuna tumia kisu kukata masega (usisahau
    kuachia nyuki robo ya mavuno ndani ya mzinga) na
    hakikisha nyuki wamepanguswa kwenye sega.
  7. g)  Hifadhi asali iliyovunwa sehemu isiyo na unyevu
    nyevu au joto kali.
UFUGAJI NYUKI
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA UVUNAJI WA ASALI
  • Usisimame katika njia wanayotumia nyuki yaani mbele
    ya mlango wa mzinga.
  • Usipakue asali wakati wa joto, jua kali au wakati mvua
    ikinyesha.
  • Unapovuna asali hakikisha umevaa mavazi ya kinga
    pia andaa zana za kumhudumia nyuki kama bomba la
    moshi.
  • Fanya kazi kwa utulivu bila ya kelele ya aina yeyote.
  • Fanya kazi kwa haraka lakini kwa uangalifu.
  • Tumia bomba la moshi kufukiza moshi ndani ya mzinga
    kwa uangalifu kisha fukiza moshi juu ya viunzi ndani ya
    mzinga.
  • Ondosha kiunzi au viunzi vichache vilivyo tupu ili
    kuweka uwazi mwishoni mwa mzinga upande mmoja. Kitendo hiki kisiwabughudhi nyuki na anza kusogeza kiunzi kimoja kimoja kwa lengo la kukagua au kuvuna asali na endelea kutumia bomba la moshi.
  • Hakikisha unarudisha kiunzi kama kilivyokuwa katika mzinga bila ya kuwadhuru nyuki.
  • Mwisho kabisa kwa taratibu rudisha mfuniko juu ya mzinga. 

JUMLA YA MIZINGA 1,400 YA NYUKI YATUNDIKWA NCHINI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. M. K Tarishi akihutubia wananchi wa wilayani Mlela mkoani Katavi (hawako pichani) katika kilele cha Siku ya taifa ya kutundika mizinga Machi 18, Mwaka huu.
Mlele, Katavi
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu imewezesha kila mkoa nchini kutundika mizinga 50 katika kuazimisha Siku ya Kutundika Mizinga kitaifa iliyofanyika Machi 18, Mwaka huu.
Akizungumza wilayani hapa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. M.K Tarishi alisema siku hii inaadhimishwa kitaifa katika Msitu wa Mlele Wilaya ya Mlele na mikoa yote Tanzania Bara inaadhimisha katika ngazi ya Mkoa kwa kutundika jumla ya mizinga 1,400 katika sehemu mbalimbali za mikoa husika.
Aliongeza kuwa Mizinga hiyo imekabidhiwa kwa vikundi vya ufugaji nyuki ili iwe ni chachu ya kuendeleza ufugaji Nyuki kwa kutumia mbinu bora za ufugaji Nyuki unaolenga kumfanya mfugaji aweze kufuga kibiashara ambapo atatakiwa kuwa na mizinga yenye makundi ya Nyuki isiyopungua 30 ambayo ndiyo yenye tija kibiashara.
Alisisitiza kuwa ufugaji wa kibiashara unamfanya mfugaji aweze kuzalisha kiasi cha kilo 450 kwa msimu chenye thamani ya Tshs. 1,500,000 na nta kilo 30 ambazo zina thamani ya Tshs. 150,000 ambayo ni mara mbili na nusu kwa wastani wa pato la mtazania.
Tathimini ya Siku ya Kutundika Mizinga mwaka jana inaonesha kuongezeka mwitikio wa jamii katika Ufugaji Nyuki. Uzalishaji wa asali umeongezeka kutoka tani 9,800 za asali na nta tani 625 kwa mwaka 2012/2013 hadi tani 19,000 za asali na tani 1,200 za nta kwa mwaka 2013/2014.
“Thamani ya kiasi hicho cha uzalishaji katika ngazi ya mfugaji ni sawa na billion 66.5. Lengo ni kuongeza uzalishaji kwa asilimia 50 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano ijayo,” Alisema Bi. Tarishi.
Wakati huo huo, Wakala wa Huduma za Misitu imeanzisha mkakati wa uzalishaji wa makundi kwa kutumia uzalishaji wa malkia ili kuhakikisha mizinga inakuwa na Nyuki badala ya kusubiria makundi yaingie yenyewe kwenye mzinga.
Akielezea kuhusu Mkakati huo, Bi. Tarishi alisema Mafunzo ya uzalishaji wa malkia na usimamzi wa makundi ya nyuki yalianza tokea mwaka 2013 yakishirikisha wataalamu 47 kutoka Kanda saba za Wakala na wafugaji nyuki 10 ambao walifanya mafunzo hayo kwa vitendo.
Alisema jumla ya malkia 120 wamezalishwa kwa kipindi cha miaka miwili cha mafunzo kwa lengo la kusambaza elimu hiyo ya uzalishaji wa malkia nchini.

Hata hivyo, alisema pamoja na ongezeko hilo uzalishaji bado ni mdogo (14%) ukilinganisha na uwezo wa nchi yetu wa kuzalisha tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka. 
Aliongeza kuwa katika kuboresha tasnia ya ufugaji nyuki ni kuwawezesha wafugaji kuwa na umoja wao ili kurahisisha huduma za ughani, kukabiliana na changamoto za masoko na kudhibiti ubora wa mazao ya nyuki.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt Rajabu Rutengwe alisema mkoa wake utahakikisha katika kila halmashauri ya mkoa kunakuwa na kituo cha kukusanyia asali ili kuweza kuthibiti ubora wa asali kwa kupima asali hiyo.
“Nimeshaagiza kila halamashauri kuhakikisha imetenga bajeti ya kuanzisha kituo cha kukusanyia asali ili kuweza kupata asali bora na uhakika wa soko kwa wafugaji nyuki, utekelezaji wa suala hili utaanza mara moja katika mwaka ujao wa fedha katika kuhakikisha wananchi wa Katavi wanajiongezea kipato, lishe, dawa na kuhifadhi mazingira,” alisema Dkt. Rutengwe.

Kaulimbiu ya siku ya taifa ya kutundika mizinga mwaka huu ni ilikuwa “BORESHA UFUGAJI NYUKI LINDA UBORA WA MAZAO YAKE”. Kauli mbiu iliyoenda pamoja na MKUKUTA II unaosisitiza kuondoa umasikini kwa wananchi na kuchangia katika pato la Taifa.

Jumatano, 26 Machi 2014

YAFAHAMU MAZAO YA NYUKI NA MATUMIZI YAKE


Mzao makuu ya nyuki ni pamoja na asali, nta, chavua, gundi ya nyuki na sumu ya nyuki.
ASALI (HONEY)
Asali hutengenezwa na nyuki kwa ajili ya chakula cha akiba.
Asali hutokana na maji matamu anayochukua nyuki kutoka kwenye maua. Wakati nyuki akikusanya maji hayo matamu yanakuwa na asilimia 20-40 ya sukari. Asilimia iliyobaki ni maji.

Asilimia hizo hupunguzwa au kuongezwa na nyuki akitumia madawa yatokayo kwenye matezi yake. Asali iliyoiva ina sukari asilimia 75-85 na maji asilimia 17-20.
Asali hutofautiana rangi, ladha vinyumbulisho kutegemeana na aina za maua aliyotembelea.
Faida za asali ni pamoja na matumizi ya nyumbani kama lishe, hutumika kama dawa pia kuboresha kipato cha mfugaji nyuki. Asali ni dawa kwa magonjwa mengi .


image.jpeg

NTA (BEESWAX)
Nta ni zao la nyuki litokalo katika mwili wa nyuki kwenye matezi yaliyopo katika sehemu ya chini ya tumbo la nyuki kibarua. Halitoki kwenye mimea kama wengi wanavyofikiria.
Kabla ya kutoa nta nyuki kibarua hutakiwa kula asali na kukaa kwa muda wa masaa 24. Matezi hutoa nta ambayo hukusanywa kwa kupelekwa mdomoni kutafunwa / kufinyangwa na kutengenezwa masega. Faida kubwa za zao la nta ni kuongeza kipato cha mfugaji nyuki kwa kuuza zao lenyewe na bidhaa zitokanazo na matumizi ya nta kama mishumaa, polishi ya samani, viatu na kadhalika.

image.jpeg

CHAVUA (POLLEN)
Chavua ni zao la nyuki kutoka kwenye mimea na ni chakula kinachompatia nyuki protein. Nyuki hukusanya chavua anapotembelea maua. Chavua hujishikiza kwenye vinyweleo vyake vya mwilini na sehemu za miguuni. Chavua hukusanywa kutoka kwenye vinyweleo vya mwili kwa miguu ya mbele hadi kufikia miguu ya nyuma yenye kipepeo. Mahitaji ya kundi la nyuki ni kama kiligram 35-40 za chavua kwa mwaka kutokana na ukubwa wa kundi la nyuki.