Nyuki vibarua ni majike kama alivyo nyuki malkia isipokuwa kutokana na tofauti ya chakula wanacholishwa wakiwa na umri mdogo (kuanzia yai-hadi kuanguliwa) hawana uwezo wa kutaga mayai. Huishi wastani wa siku 60. nyuki vibarua ndio wenye jukumu la kufanya kazi zote ndani ya mzinga.
- Usafi ndani ya mzinga.
- Kulisha majana na malkia.
- Kukusanya chavua na maji matamu.
- Ulinzi wa kundi zima, pamoja na akiba ya chakula.
- Utafutaji wa malezi mapya.
Kazi ya nyuki dume ndani ya mzinga ni kujamiana na malkia wakati mwingine husaidia katika kuongeza joto katika kiota cha majana, (brood) na anaishi wastani wa siku 120.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni