Ijumaa, 3 Januari 2014
Manufaa ya mazao ya nyuki Kijamii
Manufaa ya kijamii ya kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki hutokana na kuhamasisha umma kuhusu uwezo wa uzalishaji uliopo. Uwezekano wa maisha bora zaidi utakuwepo. Hii ni pamoja na kazi zinazohusiana na uzalishaji, uchakataji, uhifadhi, usafirishaji na masoko ya asali na nta yenye viwango bora. Kutakuwa na kazi zaidi katika shughuli za kuongeza thamani kwa mazao hayo kama vile:-
a) Vyakula vyenye asali, bia, mvinyo na madawa; na
b) Njia nyingi zaidi za kutumia nta kwa mfano utengenezaji mishumaa, batiki, pipi za
kutafuna, vipodozi vya nywele n.k.
Nyingi ya kazi hizi zitafanywa na wanawake na vijana na hii itasaidia kupunguza umaskini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni